Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 118 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ بِطَانَةٗ مِّن دُونِكُمۡ لَا يَأۡلُونَكُمۡ خَبَالٗا وَدُّواْ مَا عَنِتُّمۡ قَدۡ بَدَتِ ٱلۡبَغۡضَآءُ مِنۡ أَفۡوَٰهِهِمۡ وَمَا تُخۡفِي صُدُورُهُمۡ أَكۡبَرُۚ قَدۡ بَيَّنَّا لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡقِلُونَ ﴾
[آل عِمران: 118]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تتخذوا بطانة من دونكم لا يألونكم خبالا ودوا﴾ [آل عِمران: 118]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, msiwafanye makafiri kuwa ni wategemewa, kinyume cha Waumini, mkawa mnawapa siri zenu. Kwani wao hawakomi kuziharibu hali zenu, na wanayafurahia madhara na maovu yanayowafika. Zimedhihiri chuki nyingi katika maneno yao. Na yanayofichwa na nyoyo zao ya uadui kwenu ni makubwa zaidi na ni mazito. Kwa hakika, tushawaelezea nyinyi alama na hoja za uovu wao ili mpate kuwaidhika na muwe na tahadhari, iwapo mnayatia akilini mawaidha ya Mwenyezi Mungu, amri Zake na makatazo Yake |