Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 125 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿بَلَىٰٓۚ إِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ وَيَأۡتُوكُم مِّن فَوۡرِهِمۡ هَٰذَا يُمۡدِدۡكُمۡ رَبُّكُم بِخَمۡسَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ مُسَوِّمِينَ ﴾
[آل عِمران: 125]
﴿بلى إن تصبروا وتتقوا ويأتوكم من فورهم هذا يمددكم ربكم بخمسة آلاف﴾ [آل عِمران: 125]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ndio, unawatosha nyinyi msaada huu. Na kuna bishara nyingine kwenu, iwapo mtakuwa na subira ya kupambana na maadui zenu na mkamuogopa Mwenyezi Mungu kwa kuyatenda Aliyowamrisha na kuyaepuka Aliyowakataza. Na watakuja makafiri wa Maka kwa haraka kupigana na nyinyi, wakidhani kwamba wao watawamaliza. Mwenyezi Mungu Atawapa nyinyi msaada wa Malaika elfu tano wakiwa wamejitia alama zilizo wazi, wao na farasi wao |