Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 169 - آل عِمران - Page - Juz 4
﴿وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتَۢاۚ بَلۡ أَحۡيَآءٌ عِندَ رَبِّهِمۡ يُرۡزَقُونَ ﴾
[آل عِمران: 169]
﴿ولا تحسبن الذين قتلوا في سبيل الله أمواتا بل أحياء عند ربهم﴾ [آل عِمران: 169]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala usidhani, ewe Mtume, kwamba wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu hawahisi chochote. Bali wao wako hai uhai wa barzakh kwenye ujirani wa Mola wao Ambaye walipigana jihadi kwa ajili Yake na wakafa katika njia Yake, inawapitia riziki yao huko Peponi na wananeemeshwa |