Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 45 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿إِذۡ قَالَتِ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَٰمَرۡيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٖ مِّنۡهُ ٱسۡمُهُ ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ وَجِيهٗا فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ ﴾
[آل عِمران: 45]
﴿إذ قالت الملائكة يامريم إن الله يبشرك بكلمة منه اسمه المسيح عيسى﴾ [آل عِمران: 45]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kadhalika hukuwako huko, ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, pindi Malaika waliposema, «Ewe Maryam, Mwenyezi Mungu Anakubashiria mtoto ambaye kupatikana kwake kutatokana na neno la Mwenyezi Mungu, yaani Atamwambia, ‘Kuwa,’ na atakuwa, jina lake ni Al-Masīḥ ‘Īsā mwana wa Maryam. Yeye atakuwa na jaha katika ulimwengu na Akhera na atakuwa ni miongoni mwa wenye kukurubishwa kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama |