Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 46 - آل عِمران - Page - Juz 3
﴿وَيُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗا وَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ﴾
[آل عِمران: 46]
﴿ويكلم الناس في المهد وكهلا ومن الصالحين﴾ [آل عِمران: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na atasema na watu na hali yeye ni mtoto mchanga wa kunyonya kabla hajafikia wakati wa kusema. Na atawaita wao kwa Mwenyezi Mungu, akiwa mkubwa wakati ambapo nguvu zake zitakuwa zimeshikana na ubarobaro wake umekamilika, kwa yale aliyoletewa wahyi na Mwenyezi Mungu. Kusema huku ni kuhusu utume, ulinganizi na uongozi. Na yeye anahesabiwa kuwa ni mmoja wa watu wema na wenye utukufu wa maneno na vitendo |