×

Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, 3:84 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:84) ayat 84 in Swahili

3:84 Surah al-‘Imran ayat 84 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 84 - آل عِمران - Page - Juz 3

﴿قُلۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَمَآ أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمۡ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ ﴾
[آل عِمران: 84]

Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل آمنا بالله وما أنـزل علينا وما أنـزل على إبراهيم وإسماعيل وإسحاق, باللغة السواحيلية

﴿قل آمنا بالله وما أنـزل علينا وما أنـزل على إبراهيم وإسماعيل وإسحاق﴾ [آل عِمران: 84]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Waambie, ewe Mtume, «Tumemuamini Mwenyezi mungu na tumetii. Hatuna Mola isipokuwa Yeye, na hatuna muabudiwa isipokuwa Yeye. Tumeuamini wahyi Aliouteremsha kwetu na ule Aliouteremsha kwa Ibrāhīm aliye rafiki halisi wa Mwenyezi Mungu, na wanawe wawili, Ismā'il na Is’ḥāq, na mwana wa mwanawe,Ya'qūb mwana wa Is’ḥāq, na Asbāṭ: nao ni Manabii waliokuwa katika makabila kumi na mbili wanaotokana na watoto wa Ya'qūb, na wahyi uliopewa Mūsā na ‘Īsā wa Taurati na Injili, na wahyi Aliouteremsha Mwenyezi Mungu kwa Manabii Wake. Tunayaamini hayo yote. Wala hatumbagui yoyote katika wao. Na sisi tunamfuata Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa kumtii na kumuabudu, tunakiri Kwake kuwa Yeye Ndiye Mola, Ndiye Mungu na Ndiye wa kuabudiwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek