×

Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo 3:83 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah al-‘Imran ⮕ (3:83) ayat 83 in Swahili

3:83 Surah al-‘Imran ayat 83 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah al-‘Imran ayat 83 - آل عِمران - Page - Juz 3

﴿أَفَغَيۡرَ دِينِ ٱللَّهِ يَبۡغُونَ وَلَهُۥٓ أَسۡلَمَ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ طَوۡعٗا وَكَرۡهٗا وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ ﴾
[آل عِمران: 83]

Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: أفغير دين الله يبغون وله أسلم من في السموات والأرض طوعا وكرها, باللغة السواحيلية

﴿أفغير دين الله يبغون وله أسلم من في السموات والأرض طوعا وكرها﴾ [آل عِمران: 83]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Je, wanataka hawa wenye kutoka nje ya twaa ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa Watu wa Kitabu, dini isiyokuwa dini ya Mwenyezi Mungu nayo ni Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Alimtumiliza nao Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, hali ya kuwa wote walioko mbinguni na ardhini wamejisalimisha na kufuata na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu kwa hiyari, kama walivyo Waumini, na kwa kulazimika wakati wa shida ambapo hilo haliwanufaishi, nao ni makafiri, kama vilivyonyenyekea Kwake viumbe vyote. Na Kwake watarejeshwa Siku ya Marejeo, na alipwe kila mmoja kwa amali yake? Hili ni onyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa yoyote, katika viumbe Vyake, atakayerudi Kwake juu ya mila isiyokuwa ya Kiislamu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek