Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 27 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَهُوَ ٱلَّذِي يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَهُوَ أَهۡوَنُ عَلَيۡهِۚ وَلَهُ ٱلۡمَثَلُ ٱلۡأَعۡلَىٰ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ﴾
[الرُّوم: 27]
﴿وهو الذي يبدأ الخلق ثم يعيده وهو أهون عليه وله المثل الأعلى﴾ [الرُّوم: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anayeanzisha uumbaji viumbe kutoka kwenye hali ya kutokuwako, kisha Atawarudisha wakiwa hai baada ya kufa. Na kuwarudishia viumbe uhai baada ya kufa ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kuanzisha kuwaumba, na yote mawili ni rahisi Kwake. Na ni ya Mwenyezi Mungu sifa ya hali ya juu katika kila anachosifiwa, Hakuna chochote mfano Wake, na Yeye Ndiye Mwenye kusikia, Ndiye Mwenye kuona, Na Yeye Ndiye Mshindi Asiyeshindwa, Ndiye Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake na uendeshaji mambo ya viumbe Vyake |