Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 32 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿مِنَ ٱلَّذِينَ فَرَّقُواْ دِينَهُمۡ وَكَانُواْ شِيَعٗاۖ كُلُّ حِزۡبِۭ بِمَا لَدَيۡهِمۡ فَرِحُونَ ﴾
[الرُّوم: 32]
﴿من الذين فرقوا دينهم وكانوا شيعا كل حزب بما لديهم فرحون﴾ [الرُّوم: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na msiwe ni miongoni mwa washirikina na watu wa (kufuata) matamanio na mambo ya uzushi, walioibadilisha dini yao na wakaigeuza kwa kuchukuwa baadhi yake na kuacha baadhi yake kwa kufuata matamanio yao, wakawa ni makundi na mapote, wanafuata mikao ya viongozi wao na vyama vyao na maoni yao, wanasaidiana wao kwa wao katika batili, kila watu wa kundi wanashangilia na kufurahia mkao wao, wanajihukumia wenyewe kuwa wao wako kwenye haki na wasiokuwa wao wako kwenye ubatilifu |