Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 46 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿وَمِنۡ ءَايَٰتِهِۦٓ أَن يُرۡسِلَ ٱلرِّيَاحَ مُبَشِّرَٰتٖ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحۡمَتِهِۦ وَلِتَجۡرِيَ ٱلۡفُلۡكُ بِأَمۡرِهِۦ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴾
[الرُّوم: 46]
﴿ومن آياته أن يرسل الرياح مبشرات وليذيقكم من رحمته ولتجري الفلك بأمره﴾ [الرُّوم: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu zenye kuonyesha kuwa Yeye ndiye Mungu wa kweli Peke Yake, Asiye na Mshirika, na kuwa Ana uweza mkubwa, ni kule kutuma upepo mbele ya mvua ukiwa ni wenye kuleta habari njema, kwa kuyasukuma mawingu, hapo nafsi zikaingiwa na furaha kwa hilo, ili awaonjeshe rehema Yake kwa kuwateremshia mvua ambayo kwayo miji inahuika na pia waja, na ili jahazi zitembee baharini kwa amri Yake na matakwa Yake, na ili mtafute fadhila Zake kwa kufanya biashara na megineyo. Mwenyezi Mungu Amefanya hayo yote ili mzishukuru neema Zake na mmuabudu Yeye Peke Yake |