Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 52 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿فَإِنَّكَ لَا تُسۡمِعُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَلَا تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا وَلَّوۡاْ مُدۡبِرِينَ ﴾
[الرُّوم: 52]
﴿فإنك لا تسمع الموتى ولا تسمع الصم الدعاء إذا ولوا مدبرين﴾ [الرُّوم: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika wewe, ewe Mtume, humsikilizishi yule ambaye moyo wake umekufa au mashikio yake yamezibana yakawa hayaisikii haki. Basi usibabaike wala usisikitike kwa kukataa kukuamini hawa washirikina, kwani wao ni kama viziwi na wafu, hawasikii wala hawahisi hata kama wako mbele yako, basi itakuwa vipi iwapo hawako na wewe na wamekupa mgongo |