Quran with Swahili translation - Surah Luqman ayat 20 - لُقمَان - Page - Juz 21
﴿أَلَمۡ تَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَأَسۡبَغَ عَلَيۡكُمۡ نِعَمَهُۥ ظَٰهِرَةٗ وَبَاطِنَةٗۗ وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَلَا هُدٗى وَلَا كِتَٰبٖ مُّنِيرٖ ﴾
[لُقمَان: 20]
﴿ألم تروا أن الله سخر لكم ما في السموات وما في الأرض﴾ [لُقمَان: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hamuoni, enyi watu, kuwa Mwenyezi Mungu amewadhalilishia vilivyoko mbinguni miongoni mwa jua, mwezi, mawingu na vinginevyo, na vilivyoko ardhini miongoni mwa wanyama, miti, maji na vinginevyo visivyodhibitika, na Akaeneza kwenu neema Zake za nje juu ya miili na viungo, na za ndani, kwenye akili na nyoyo, na zile Alizowawekea katika zile msizozijua? Na miongoni mwa watu kuna anayefanya ushindani juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada bila ya hoja wala ubainifu wala kitabu chenye kubainisha kinachofafanua uhakika wa madai yako |