Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 13 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِي لِأَجَلٖ مُّسَمّٗىۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۚ وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ مَا يَمۡلِكُونَ مِن قِطۡمِيرٍ ﴾
[فَاطِر: 13]
﴿يولج الليل في النهار ويولج النهار في الليل وسخر الشمس والقمر كل﴾ [فَاطِر: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Anazitia nyakati za usiku ndani mchana, hivyo basi mchana ukarefuka kwa kadiri ya usiku uliopungua; na Anazitia nyakati za mchana ndani ya usiku, hivyo basi usiku ukarefuka kwa kadiri ya mchana uliopungua. Na Amedhalilisha jua na mwezi vikawa vinatembea kwa wakati maaalumu. Huyo aliyefanya hili ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Ni Wake Yeye ufalme wote. Na wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawamiliki hata utandu mwembamba unaozunguka koko ya tende |