Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 8 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿أَفَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ فَرَءَاهُ حَسَنٗاۖ فَإِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۖ فَلَا تَذۡهَبۡ نَفۡسُكَ عَلَيۡهِمۡ حَسَرَٰتٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ ﴾
[فَاطِر: 8]
﴿أفمن زين له سوء عمله فرآه حسنا فإن الله يضل من يشاء﴾ [فَاطِر: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, yule ambaye Shetani anampambia matendo yake maovu ya kumuasi Mwenyezi Mungu, kukufuru na kuwaabudu wasiyekuwa Yeye miongoni mwa waungu na masanamu, akayaona ni mazuri yenye kupendeza, (Je, yeye) ni kama yule ambaye Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amemuongoza akaliona zuri kuwa ni zuri na ovu kuwa ni ovu? Hakika Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayemtaka na Anamuongoza Anayemtaka. Basi usijiangamize kwa kuwa na huzuni juu ya ukanushaji wa hawa waliopotea. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua maovu yao na Atawalipa kwa hayo malipo mabaya kabisa |