Quran with Swahili translation - Surah Ya-Sin ayat 41 - يسٓ - Page - Juz 23
﴿وَءَايَةٞ لَّهُمۡ أَنَّا حَمَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُمۡ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ ﴾
[يسٓ: 41]
﴿وآية لهم أنا حملنا ذريتهم في الفلك المشحون﴾ [يسٓ: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ushahidi na hoja kwao kwamba Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa, Ndiye mneemeshaji neema nyingi, ni kwamba sisi tuliwabeba wale waliookoka miongoni mwa wanadamu katika jahazi la Nūḥ lililojazwa jinsi mbalimbali ya viumbe, ili maisha yaendelee baada ya mafuriko |