Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 104 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَلَا تَهِنُواْ فِي ٱبۡتِغَآءِ ٱلۡقَوۡمِۖ إِن تَكُونُواْ تَأۡلَمُونَ فَإِنَّهُمۡ يَأۡلَمُونَ كَمَا تَأۡلَمُونَۖ وَتَرۡجُونَ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا يَرۡجُونَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴾
[النِّسَاء: 104]
﴿ولا تهنوا في ابتغاء القوم إن تكونوا تألمون فإنهم يألمون كما تألمون﴾ [النِّسَاء: 104]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala msiwe walegevu katika kuwatafuta maadui wenu na kupigana nao. Mkiwa mnahisi uchungu wa vita na matokeo yake, basi maadui wenu pia wanahisi uchungu wake zaidi, na pamoja na hivyo, hawakomi kupigana nanyi. Basi nyinyi ni aula kwa hilo kuliko wao, kwa kuwa nyinyi mnatarajia thawabu, nusura na kupewa nguvu, na wao hawatarajii hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali zenu zote, ni Mwenye hekima katika maamrisho Yake na uendeshaji mambo Wake |