Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 116 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا ﴾
[النِّسَاء: 116]
﴿إن الله لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن﴾ [النِّسَاء: 116]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hasamehe Akishirikishwa na Anasamehe madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliye Mmoja, Aliye Pekee, mshirika yoyote, miongoni mwa waja Wake, atakuwa yuko mbali sana na haki |