×

Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao 4:128 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:128) ayat 128 in Swahili

4:128 Surah An-Nisa’ ayat 128 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 128 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿وَإِنِ ٱمۡرَأَةٌ خَافَتۡ مِنۢ بَعۡلِهَا نُشُوزًا أَوۡ إِعۡرَاضٗا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يُصۡلِحَا بَيۡنَهُمَا صُلۡحٗاۚ وَٱلصُّلۡحُ خَيۡرٞۗ وَأُحۡضِرَتِ ٱلۡأَنفُسُ ٱلشُّحَّۚ وَإِن تُحۡسِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 128]

Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإن امرأة خافت من بعلها نشوزا أو إعراضا فلا جناح عليهما أن, باللغة السواحيلية

﴿وإن امرأة خافت من بعلها نشوزا أو إعراضا فلا جناح عليهما أن﴾ [النِّسَاء: 128]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na mwanamke akijua kuwa mumewe ana majivuno na madharau na hashughuliki naye, si makosa kwa wao wawili kusikilizana kwa namana ya kuwaridhisha wao wawili kuhusu kugawa siku na matumizi. Kwani masikilizano ni bora zaidi na ni afadhali zaidi. Na nafsi zimeumbwa zikiwa na tabia ya pupa na ubahili, kama kwamba ubahili upo mbele ya hizo nafsi, hauepukani nazo. Na mkiamiliana na wake wenu vizuri na mkamcha Mwenyezi Mungu juu yao, basi Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa mnayoyafanya, katika hayo na mengineyo, hakuna kinachofichika Kwake, na Atawalipa kwa hayo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek