Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 129 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَلَن تَسۡتَطِيعُوٓاْ أَن تَعۡدِلُواْ بَيۡنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوۡ حَرَصۡتُمۡۖ فَلَا تَمِيلُواْ كُلَّ ٱلۡمَيۡلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلۡمُعَلَّقَةِۚ وَإِن تُصۡلِحُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 129]
﴿ولن تستطيعوا أن تعدلوا بين النساء ولو حرصتم فلا تميلوا كل الميل﴾ [النِّسَاء: 129]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hamtaweza, enyi wanaume, kuhakikisha uadilifu kamili wa mapenzi na muelekeo wa moyo kati ya wanawake, namna mtakavyofanya bidii juu ya hilo. Basi msimpe mgongo, yule msiokuwa na haja naye, kabisa-kabisa mkamuacha akawa ni kama mwanamke ambaye hana mume wala hakutalikiwa, mkaja mkapata madhambi. Na mkizitengeneza amali zenu mkafanya uadilifu katika ugawaji wenu baina ya wake zenu na mkamchunga Mwenyezi Mungu mkamuogopa juu yao, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao |