Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 150 - النِّسَاء - Page - Juz 6
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤۡمِنُ بِبَعۡضٖ وَنَكۡفُرُ بِبَعۡضٖ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُواْ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴾
[النِّسَاء: 150]
﴿إن الذين يكفرون بالله ورسله ويريدون أن يفرقوا بين الله ورسله ويقولون﴾ [النِّسَاء: 150]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika wanaomkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, kati ya Mayahudi na Wanaswara, na kutaka kutenganisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, kwa kumuamini kwao Mwenyezi Mungu na kuwakanusha Mitume Wake Aliowatuma kwa viumbe Wake, au wautambue ukweli wa baadhi ya Mitume na kuacha kuwatambua wengine na wadai kwamba baadhi yao wamemzulia Mola wao urongo na wanataka kujifanyia njia ya kuelekea kwenye upotofu waliouanzisha na uzushi waliouzua |