Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 19 - النِّسَاء - Page - Juz 4
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَحِلُّ لَكُمۡ أَن تَرِثُواْ ٱلنِّسَآءَ كَرۡهٗاۖ وَلَا تَعۡضُلُوهُنَّ لِتَذۡهَبُواْ بِبَعۡضِ مَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِن كَرِهۡتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَيَجۡعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيۡرٗا كَثِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 19]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا يحل لكم أن ترثوا النساء كرها ولا تعضلوهن﴾ [النِّسَاء: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mlioamini, haifai kwenu kuwafanya wake wa baba zenu ni miongoni mwa mali yalioachwa kurithiwa, mkawa mnafanya mtakavyo kwao: kwa kuwaoa, kuwakataza wasiolewe au kuwaoza waume wengine, hali ya kuwa wao hawayataki hayo yote. Na pia haifai kwenu kuwadhuru wake zenu kwa kuwa mnawachukia, ili wapate kusamehe baadhi ya mlivyowapa, mahari au vinginevyo. Isipokuwa wakiwa wamefanya jambo ovu, kama uzinifu, hapo mnayo nafasi ya kuwazuia mpaka mkitwae mlichowapa. Na kule kukaa kwenu na wake zenu yatakikana kuwe ni juu ya misingi ya heshima na mapenzi na kuwatekelezea haki zao. Na iwapo mtawachukia kwa sababu yoyote katika sababu za kidunia, basi kuweni na subira. Kwani huenda mkachukia jambo, miongoni mwa mambo, na ikawa ndani yake muna kheri nyingi |