Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 2 - النِّسَاء - Page - Juz 4
﴿وَءَاتُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰٓ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَتَبَدَّلُواْ ٱلۡخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِۖ وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَهُمۡ إِلَىٰٓ أَمۡوَٰلِكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبٗا كَبِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 2]
﴿وآتوا اليتامى أموالهم ولا تتبدلوا الخبيث بالطيب ولا تأكلوا أموالهم إلى أموالكم﴾ [النِّسَاء: 2]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale waliofiliwa na baba zao wakiwa bado hawajabaleghe, na mkawa nyinyi ndio wasimamizi wao, wapeni mali zao wafikapo umri wa kubaleghe, muonapo kutoka kwao kuwa wana uwezo wa kuhifadhi mali zao. Na wala msichukuwe kizuri katika mali zao na mkaweka mahali pake kibaya katika mali zenu. Wala msichanganye mali zao na mali zenu ili mpate kula mali zao kwa hila. Na mwenye kujasiri kulitenda hilo, hakika huyo amefanya dhambi kubwa |