Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 26 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمۡ وَيَهۡدِيَكُمۡ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَيَتُوبَ عَلَيۡكُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ﴾
[النِّسَاء: 26]
﴿يريد الله ليبين لكم ويهديكم سنن الذين من قبلكم ويتوب عليكم والله﴾ [النِّسَاء: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Katika kuwaekea Sheria hizi, Mwenyezi Mungu Anataka kuwafunulia wazi alama za dini Yake iliyolingana na hukumu Zake zenye hekima, kuwaonesha njia za Mitume na watu wema waliokuwa kabla yenu katika halali na haramu na kuwakubalia toba zenu kwa kuwarudisha kwenye kumtii Mwenyezi Mungu. Na Yeye, Aliyetakasika na sifa pungufu, ni Mjuzi wa yale yenye kutengeneza mambo ya waja Wake, ni Mwenye hekima katika sheria Zake Alizowaekea |