Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 38 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَهُۥ قَرِينٗا فَسَآءَ قَرِينٗا ﴾
[النِّسَاء: 38]
﴿والذين ينفقون أموالهم رئاء الناس ولا يؤمنون بالله ولا باليوم الآخر ومن﴾ [النِّسَاء: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pia tumewaandalia adhabu hii wale ambao wanatoa mali yao kwa njia ya ria na kujitangaza na hawamuamini Mwenyezi Mungu, kiitikadi na kivitendo, wala Siku ya Kiyama. Matendo haya mabaya ni miongoni mwa yale yanayolinganiwa na Shetani. Na yoyote yule ambaye Shetani atakuwa ni mwenye kushikamana na yeye, basi mtu mbaya wa kushikamana naye na kufanya naye urafiki ni yeye |