×

Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala 4:43 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:43) ayat 43 in Swahili

4:43 Surah An-Nisa’ ayat 43 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 43 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡرَبُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمۡ سُكَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعۡلَمُواْ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغۡتَسِلُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴾
[النِّسَاء: 43]

Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba - isipo kuwa mmo safarini - mpaka mkoge. Na mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake - na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kughufiria

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا لا تقربوا الصلاة وأنتم سكارى حتى تعلموا ما تقولون, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا لا تقربوا الصلاة وأنتم سكارى حتى تعلموا ما تقولون﴾ [النِّسَاء: 43]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Yake kivitendo, msiikaribie Swala wala msisimame kwenda kusali mkiwa katika hali ya ulevi mpaka muyaelewe na muyajue mnayoyasema. -Hii ilikuwa kabla ya kuthibitishwa uharamu wa pombe katika hali zote-.Na wala msikaribie Swala mkiwa na hadathi kubwa, nayo ni janaba. Na pia, mkiwa na janaba, msizikaribe sehemu za Swala, nazo ni misikiti, isipokuwa kwa mpita njia, katika nyinyi, kutoka kwenye mlango hadi mlango mwingine, mpaka mjitwahirishe kwa kuoga. Na mkiwa katika hali ya ugonjwa, mkawa hamuwezi kutumia maji, au hali ya safari, au mmoja wenu akaja kutoka kwenye haja kubwa au ndogo au mkawaingilia wanawake na msipate maji ya kujisafisha, ujieni mchanga uliyo tohara mjipanguse nao nyuso zenu na mikono yenu. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Anayasamehe makosa yenu na Anawasitiria
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek