Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 58 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿۞ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُكُمۡ أَن تُؤَدُّواْ ٱلۡأَمَٰنَٰتِ إِلَىٰٓ أَهۡلِهَا وَإِذَا حَكَمۡتُم بَيۡنَ ٱلنَّاسِ أَن تَحۡكُمُواْ بِٱلۡعَدۡلِۚ إِنَّ ٱللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا ﴾
[النِّسَاء: 58]
﴿إن الله يأمركم أن تؤدوا الأمانات إلى أهلها وإذا حكمتم بين الناس﴾ [النِّسَاء: 58]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Anawaamrisha nyinyi kutekeleza aina zote za amana mlizoaminiwa nazo kwa wenyewe, msizifanyie dharau. Na Anawaamrisha muhukumu baina ya watu kwa uadilifu na uhaki, mtakapohukumu baina yao.Hilo ni jambo bora zaidi Analowaidhia Mwenyezi Mungu na kuwaongoza mlifanye. Hakika Mweyezi Mungu Aliyetukuka ni Msikizi wa maneno yenu, Anayajua matendo yenu na Anayaona |