×

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka 4:59 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:59) ayat 59 in Swahili

4:59 Surah An-Nisa’ ayat 59 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 59 - النِّسَاء - Page - Juz 5

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَأُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنكُمۡۖ فَإِن تَنَٰزَعۡتُمۡ فِي شَيۡءٖ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلًا ﴾
[النِّسَاء: 59]

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا أطيعوا الله وأطيعوا الرسول وأولي الأمر منكم فإن تنازعتم, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا أطيعوا الله وأطيعوا الرسول وأولي الأمر منكم فإن تنازعتم﴾ [النِّسَاء: 59]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, zikubalini amri za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na wala msimuasi, mkubalini Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kwa yale Aliyokuja nayo ya haki na watiini watawala wa mambo yenu isipokuwa katika kumuasi Mwenyezu Mungu. Na mnapotafautiana baina yenu katika kitu chochote, basi irudisheni hukumu yake kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Sunnah ya Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, iwapo nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Siku ya Mwisho Imani ipasavyo. Kurudisha huko kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ni bora kwenu kuliko kubishana na kusema kwa maoni, na ni mazuri kabisa marejeo yake na mwisho wake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek