Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 95 - النِّسَاء - Page - Juz 5
﴿لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡقَٰعِدُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ غَيۡرُ أُوْلِي ٱلضَّرَرِ وَٱلۡمُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ فَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ دَرَجَةٗۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَفَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا ﴾
[النِّسَاء: 95]
﴿لا يستوي القاعدون من المؤمنين غير أولي الضرر والمجاهدون في سبيل الله﴾ [النِّسَاء: 95]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wenye kusalia nyuma wakaacha kuhudhuria jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa wenye nyudhuru kati yao, hawalingani na wenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewafadhilisha wenye kupigana jihadi juu ya wenye kukaa na Ameitukuza daraja yao Peponi kwa kiwango cha juu. Na Mwenyezi Mungu Amewaahidi wote: wenye kupigana jihadi kwa mali yao na kwa nafsi zao na wenye kukaa, miongoni mwa watu wenye nyudhuru, kwa kutoa kwao na kujitolea katika njia ya haki. Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amewafadhilisha wale wenye kupigana jihadi juu ya wenye kukaa kwa kuwapa thawabu nyingi |