Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 13 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿هُوَ ٱلَّذِي يُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ رِزۡقٗاۚ وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ ﴾
[غَافِر: 13]
﴿هو الذي يريكم آياته وينـزل لكم من السماء رزقا وما يتذكر إلا﴾ [غَافِر: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Anayewaonyesha, enyi watu, uweza Wake kwa zile alama kubwa zenye kutolea ushahidi ukamilifu wa Mwenye kuziumba na kuzianzisha, na Anawateremshia mvua kutoka mawinguni ambayo kwayo mnaruzukiwa. Na hajikumbushi kwa alama hizi isipokuwa yule anayerudi kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada |