Quran with Swahili translation - Surah Ghafir ayat 67 - غَافِر - Page - Juz 24
﴿هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ مِنۡ عَلَقَةٖ ثُمَّ يُخۡرِجُكُمۡ طِفۡلٗا ثُمَّ لِتَبۡلُغُوٓاْ أَشُدَّكُمۡ ثُمَّ لِتَكُونُواْ شُيُوخٗاۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبۡلُۖ وَلِتَبۡلُغُوٓاْ أَجَلٗا مُّسَمّٗى وَلَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ ﴾
[غَافِر: 67]
﴿هو الذي خلقكم من تراب ثم من نطفة ثم من علقة ثم﴾ [غَافِر: 67]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Aliyemuumba baba yenu Ādam kwa mchanga, kisha Akawafanya mpatikane kutokana na manii kwa uweza Wake, na baada yake mnahamia kwenye mwongo wa damu nzito iliyo nyekundu, kisha mnapitiwa na miongo kadha ndani ya vizazi, mpaka mnapozaliwa mkiwa watoto wadogo, kisha umbile lenu linapata nguvu (na mnaendelea hivyo) mpaka mnapokuwa wazee, na miongoni mwenu kuna wanaokufa kabla ya hapo. Na ili mfikie kwa miongo hii kipindi kiliotajwa ambacho hapo umri wenu ukome. Huenda nyinyi mkazitia akilini hoja za Mwenyezi Mungu katika hilo na mkazizingatia aya zake mkajua kuwa hakuna Mola isipokuwa Yeye Anayefanya hilo, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye haitakiwi kuabudiwa isipokuwa Yeye |