Quran with Swahili translation - Surah Ash-Shura ayat 15 - الشُّوري - Page - Juz 25
﴿فَلِذَٰلِكَ فَٱدۡعُۖ وَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَۖ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡۖ وَقُلۡ ءَامَنتُ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِن كِتَٰبٖۖ وَأُمِرۡتُ لِأَعۡدِلَ بَيۡنَكُمُۖ ٱللَّهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمۡۖ لَنَآ أَعۡمَٰلُنَا وَلَكُمۡ أَعۡمَٰلُكُمۡۖ لَا حُجَّةَ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُۖ ٱللَّهُ يَجۡمَعُ بَيۡنَنَاۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ ﴾
[الشُّوري: 15]
﴿فلذلك فادع واستقم كما أمرت ولا تتبع أهواءهم وقل آمنت بما أنـزل﴾ [الشُّوري: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi, kwenye dini hiyo iliyolingana sawa ambayo Mwenyezi Mungu Aliwawekea Manabii na Akawausia waifuate, lingania, ewe Mtume, waja wa Mwenyezi Mungu, na uwe na msimamo wa kisawa kama Anavyokuamrisha Mwenyezi Mungu. Na usifuate matamanio ya wale walioifanyia haki shaka na wakapotoka kwa kuwa kando na Dini, na useme, «Nimeviamini Vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka mbinguni kwa Manabiii, Na Mola wangu Ameniamrisha nifanye uadilifu baina yenu katika kuhukumu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu na Mola wenu. Sisi tutapata thawabu ya matendo yetu mema, na nyinyi mtapata malipo ya matendo yenu maovu. Hakuna utesi wala mjadala baina yetu sisi na nyinyi baada ya haki kufafanuka. Mwenyezi Mungu Atatukusanya sisi na nyinyi Siku ya Kiyama Ahukumu baina yetu kwa haki katika yale tuliyotafautiana, na kwake Yeye ndio marejeo na marudio, na huko Amlipe kila mmoja kwa anachostahiki.» |