Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 26 - الأحقَاف - Page - Juz 26
﴿وَلَقَدۡ مَكَّنَّٰهُمۡ فِيمَآ إِن مَّكَّنَّٰكُمۡ فِيهِ وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ سَمۡعٗا وَأَبۡصَٰرٗا وَأَفۡـِٔدَةٗ فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُمۡ سَمۡعُهُمۡ وَلَآ أَبۡصَٰرُهُمۡ وَلَآ أَفۡـِٔدَتُهُم مِّن شَيۡءٍ إِذۡ كَانُواْ يَجۡحَدُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ ﴾
[الأحقَاف: 26]
﴿ولقد مكناهم فيما إن مكناكم فيه وجعلنا لهم سمعا وأبصارا وأفئدة فما﴾ [الأحقَاف: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tuliwarahisishia hao 'Ād sababu za kumakinika duniani kwa namna ambayo hatukuwamakinisha nyinyi, enyi Makureshi, na tukawafanya wawe na masikio ya wao kusikia na macho ya wao kuonea na nyoyo za wao kufahamia, wakavitumia katika mambo yanayomfanya Mwenyezi Mungu Awe na hasira nao. Na hilo halikuwafalia kitu chochote kwa kuwa walikuwa wakikanusha hoja za Mwenyezi Mungu, na hiyo adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia shere na kuiharakisha. Hili ni onyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, imetukuka shani Yake, na ni tahadharisho kwa wenye kukufuru |