Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 27 - الأحقَاف - Page - Juz 26
﴿وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَا مَا حَوۡلَكُم مِّنَ ٱلۡقُرَىٰ وَصَرَّفۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ ﴾
[الأحقَاف: 27]
﴿ولقد أهلكنا ما حولكم من القرى وصرفنا الآيات لعلهم يرجعون﴾ [الأحقَاف: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tuliiangamiza miji iliyokuwa pambizoni mwenu, enyi watu wa Makkah, kama ile ya kina 'Ād na Thamūd, tukazifanya kuta za nyumba za miji hiyo zimeanguka na kulalia sakafu zake zilizovunjika, na tuliwabainishia watu wa miji hiyo aina za hoja na dalili wapate kurudi nyuma na kuyaacha yale waliokuwa nayo ya ukanushaji Mwenyezi Mungu na aya Zake |