Quran with Swahili translation - Surah Al-Ahqaf ayat 35 - الأحقَاف - Page - Juz 26
﴿فَٱصۡبِرۡ كَمَا صَبَرَ أُوْلُواْ ٱلۡعَزۡمِ مِنَ ٱلرُّسُلِ وَلَا تَسۡتَعۡجِل لَّهُمۡۚ كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَ مَا يُوعَدُونَ لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا سَاعَةٗ مِّن نَّهَارِۭۚ بَلَٰغٞۚ فَهَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ﴾
[الأحقَاف: 35]
﴿فاصبر كما صبر أولو العزم من الرسل ولا تستعجل لهم كأنهم يوم﴾ [الأحقَاف: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yanayokupata ya makero ya watu wako wenye kukukanusha kama vile walivyovumilia Mitume wenye nia thabiti kabla yako wewe, nao, kwa kauli mashuhuri, ni Nūḥ, Ibrāhīm, Mūsā na Īsā, na wewe ni miongoni mwao, wala usiwafanyie haraka watu wako ya kuadhibiwa. Kwani itapotokea na wakaiona, watajihisi kama kwamba hawakukaa duniani isipokuwa muda mchache wa mchana. Haya ni mafikisho kwao na kwa wasiokuwa wao. Na haangamizwi kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu waliotoka nie ya amri Yake na twaa Yake |