Quran with Swahili translation - Surah Muhammad ayat 3 - مُحمد - Page - Juz 26
﴿ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡبَٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡحَقَّ مِن رَّبِّهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمۡثَٰلَهُمۡ ﴾
[مُحمد: 3]
﴿ذلك بأن الذين كفروا اتبعوا الباطل وأن الذين آمنوا اتبعوا الحق من﴾ [مُحمد: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kupoteza huko na kuongoza, sababu yake ni kwamba wale waliokufuru wamemfuata Shetani wakamtii, na kwamba wale walioamini walimfuata Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo ya mwangaza na uongofu. Kama Alivyobainisha Mwenyezi Mungu vile Anavyoyafanya mapote mawili ya watu wa ukafiri na watu wa Imani kwa wanavyostahili, vilevile Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Anawapigia watu mifano yao, ili kila watu wanaofanana wa aina moja wakutamane na wale wanaonasibiana nao |