Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 15 - الفَتح - Page - Juz 26
﴿سَيَقُولُ ٱلۡمُخَلَّفُونَ إِذَا ٱنطَلَقۡتُمۡ إِلَىٰ مَغَانِمَ لِتَأۡخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعۡكُمۡۖ يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُواْ كَلَٰمَ ٱللَّهِۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمۡ قَالَ ٱللَّهُ مِن قَبۡلُۖ فَسَيَقُولُونَ بَلۡ تَحۡسُدُونَنَاۚ بَلۡ كَانُواْ لَا يَفۡقَهُونَ إِلَّا قَلِيلٗا ﴾
[الفَتح: 15]
﴿سيقول المخلفون إذا انطلقتم إلى مغانم لتأخذوها ذرونا نتبعكم يريدون أن يبدلوا﴾ [الفَتح: 15]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watasema wale walioachwa nyuma utakapoondoka, ewe Nabii, wewe na Maswahaba wako kuelekea kwenye ngawira za Khaybar ambazo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi nyinyi kuwa mtazipata, «Tuacheni tuende na nyinyi huko Khaybar» wakiwa wanataka kwa hilo kubadilisha ahadi ya Mwenyezi Mungu kwenu. Waambie, «Hamtatoka pamoja na sisi kwenda Khaybar, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Alitwambia kabla hatujarudi Madina kwamba ngawira za Khaybar ni za wale waliohudhuria Ḥudaybiyah pamoja na sisi.» Watasema, «Mambo sivyo kama mnavyosema. Mwenyezi Mungu Hakuwaamrisha nyinyi hili. Nyinyi mnatukataza kutoka na nyinyi kwa uhasidi wenu tusije tukapata ngawira pamoja na nyinyi.» Mambo sivyo kama walivyodai, bali wao walikuwa hawaelewi amri za Mwenyezi Mungu kuhusu haki zao na wajibu wao wa kidini isipokuwa kidogo |