Quran with Swahili translation - Surah Al-Fath ayat 4 - الفَتح - Page - Juz 26
﴿هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِيمَٰنٗا مَّعَ إِيمَٰنِهِمۡۗ وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا ﴾
[الفَتح: 4]
﴿هو الذي أنـزل السكينة في قلوب المؤمنين ليزدادوا إيمانا مع إيمانهم ولله﴾ [الفَتح: 4]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyeteremsha utulivu ndani ya nyoyo za wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika siku ya Ḥudaybiyah zikatulia na yakini ikajidhatititi ndani ya hizo nyoyo, ili wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Wake pamoja na kuamini kwao na kufuata kwao. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ana askari wa mbinguni na ardhini, Anawanusuru kwa askari hao waja Wake Waumini. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa maslahi ya viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na utengezaji Wake |