Quran with Swahili translation - Surah Al-hujurat ayat 14 - الحُجُرَات - Page - Juz 26
﴿۞ قَالَتِ ٱلۡأَعۡرَابُ ءَامَنَّاۖ قُل لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ وَلَٰكِن قُولُوٓاْ أَسۡلَمۡنَا وَلَمَّا يَدۡخُلِ ٱلۡإِيمَٰنُ فِي قُلُوبِكُمۡۖ وَإِن تُطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَا يَلِتۡكُم مِّنۡ أَعۡمَٰلِكُمۡ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ﴾
[الحُجُرَات: 14]
﴿قالت الأعراب آمنا قل لم تؤمنوا ولكن قولوا أسلمنا ولما يدخل الإيمان﴾ [الحُجُرَات: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waarabu wa majangwani, nao ni Mabedui, walisema, «Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Imani iliyokamilika.» Waambie, ewe Nabii, «Msijidai kuwa mna Imani kamilifu, lakini semeni, ‘Tumesilimu.’ na bado Imani haijaingia ndani ya nyoyo zenu. Na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Hatawapunguzia chochote katika thawabu za matendo yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa anayetubia dhambi zake, ni Mwingi wa rehema kwake.» Katika hii aya kuna makemeo kwa mtu anayedhihirisha kuamini na kufuata Sunnah, na hali matendo yake yanashuhudilia kinyume cha hayo |