×

Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa 5:101 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:101) ayat 101 in Swahili

5:101 Surah Al-Ma’idah ayat 101 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 101 - المَائدة - Page - Juz 7

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهَاۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ ﴾
[المَائدة: 101]

Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا لا تسألوا عن أشياء إن تبد لكم تسؤكم وإن, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا لا تسألوا عن أشياء إن تبد لكم تسؤكم وإن﴾ [المَائدة: 101]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enye ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu, Mtume wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiulize mambo ya Dini ambayo hamkuamrishwa chochote kuhusu hayo, kama kuuliza kuhusu mambo ambayo hayajatukia au yale ambayo yatapelekea mikazo ya Sheria ambayo lau mlikalifishwa nayo yangalikuwa ni magumu kwenu, na lau mliyauliza wakati wa uhai wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, wakati Qur’ani inateremka, mungalielezewa, na pengine mkakalifishwa nayo na mkalemewa nayo. Hayo Mwenyezi Mungu Ameyaacha ili kuwapumzisha waja Wake nayo. Na Mwenyezi Mungu ni Msamehefu sana kwa waja wake wanapotubia, ni Mpole sana kwao, Hawaadhibu wakirudi Kwake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek