Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 110 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱذۡكُرۡ نِعۡمَتِي عَلَيۡكَ وَعَلَىٰ وَٰلِدَتِكَ إِذۡ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِ تُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗاۖ وَإِذۡ عَلَّمۡتُكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَۖ وَإِذۡ تَخۡلُقُ مِنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِ بِإِذۡنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِيۖ وَتُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ تُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ كَفَفۡتُ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ عَنكَ إِذۡ جِئۡتَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ ﴾
[المَائدة: 110]
﴿إذ قال الله ياعيسى ابن مريم اذكر نعمتي عليك وعلى والدتك إذ﴾ [المَائدة: 110]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Atakaposema Mwenyezi Mungu, Siku ya Kiyama, «Ewe ‘Īsā mwana wa Maryam! Kumbuka neema yangu kwako, nilipokuumba bila ya baba, na kwa mamako, nilipomteua juu ya wanawake wa ulimwengu na nikamuepusha na hatia aliyobandikwa nayo.» Miongoni mwa neema hizi kwa ‘Īsā ni kwamba Mwenyezi Mungu Alimpa nguvu na Akamsaidia kwa Jibrili, amani imshukie, akasema na watu na yeye ni mchanga wa kunyonya kabla ya wakati wa kusema na akawaita wao kuja kwa Mwenyezi Mungu na yeye ni mkubwa, nguvu zake zimeshikana, na ubarobaro wake umekamilika, kwa wahyi wa tawhīd ambao Mwenyezi Mungu Alimletea. Na miongoni mwa hizo ni kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Alimfundisha kuandika na (kusoma) maandishi bila ya mwalimu, Alimpa nguvu ya kufahamu na kuelewa, Alimfundisha Taurati Aliyomteremshia Mūsā, amani imshukie, Injili Aliyomteremshia yeye ili kuwaongoza watu. Na miongoni mwa neema hizi ni kwamba yeye anasinyanga kwa udongo kama umbo la ndege na kisha anapuliza kwenye umbo hilo na likawa ni ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwazo ni kwamba yeye anamponyesha aliyezaliwa kipofu akawa anaona na anamponyesha mwenye mbalanga ikarudi ngozi yake kuwa na uzima kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwazo ni kwamba yeye anamuomba Mwenyezi Mungu Awahui wafu, na wakainuka kutoka kwenye makaburi yao wakiwa hai. Yote hayo ni kwa matakwa Mwenyezi Mungu , Aliyetukuka, na idhini Yake. Nayo ni miujiza yenye kushinda, inautilia nguvu unabii wa ‘Īsā, amani imshukie. Kisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Anamkumbusha neema Yake kwake alipowazuia Wana wa Isrāīl walipotaka kumuua na akawajia wao na miujiza iliyo wazi yenye kuonyesha dalili za unabii wake. Hapo walisema waliokufuru kati yao, «Hakika haya aliyokuja nayo ‘Īsā, miongoni mwa dalili zilizo wazi, ni uchawi uliofichuka |