Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 111 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿وَإِذۡ أَوۡحَيۡتُ إِلَى ٱلۡحَوَارِيِّـۧنَ أَنۡ ءَامِنُواْ بِي وَبِرَسُولِي قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَٱشۡهَدۡ بِأَنَّنَا مُسۡلِمُونَ ﴾
[المَائدة: 111]
﴿وإذ أوحيت إلى الحواريين أن آمنوا بي وبرسولي قالوا آمنا واشهد بأننا﴾ [المَائدة: 111]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ukumbuke, ewe ‘Īsā, nilipotia ilhamu na msukumo katika nyoyo za watu, miongoni mwa wale waliosafiwa nawe, kuwafanya wauamini upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na unabii wako, wakasema, «Tumeamini, ewe Mola wetu. Na ushuhudie kuwa sisi ni wenye kukunyenyekea na ni wenye kufuata kwa utiifu amri Yako |