Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 115 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿قَالَ ٱللَّهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيۡكُمۡۖ فَمَن يَكۡفُرۡ بَعۡدُ مِنكُمۡ فَإِنِّيٓ أُعَذِّبُهُۥ عَذَابٗا لَّآ أُعَذِّبُهُۥٓ أَحَدٗا مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ ﴾
[المَائدة: 115]
﴿قال الله إني منـزلها عليكم فمن يكفر بعد منكم فإني أعذبه عذابا﴾ [المَائدة: 115]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, aliyetukuka, Akasema, «Mimi ni Mwenye kuwateremshia Meza ya chakula. Basi yoyote mwenye kuukanusha upweke wangu, miongoni mwenu, na unabii wa ‘Īsā, amani imshukie, baada ya kuteremka meza, nitamuadhibu adhabu kali ambayo sitamuadhibu nayo yoyote miongoni mwa viumbe.» Meza iliteremka kama alivyoahidi Mwenyezi Mungu |