×

Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wa fanyao haraka kukufuru, miongoni mwa wanao sema kwa 5:41 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:41) ayat 41 in Swahili

5:41 Surah Al-Ma’idah ayat 41 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 41 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ لَا يَحۡزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡكُفۡرِ مِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَلَمۡ تُؤۡمِن قُلُوبُهُمۡۛ وَمِنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْۛ سَمَّٰعُونَ لِلۡكَذِبِ سَمَّٰعُونَ لِقَوۡمٍ ءَاخَرِينَ لَمۡ يَأۡتُوكَۖ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ مِنۢ بَعۡدِ مَوَاضِعِهِۦۖ يَقُولُونَ إِنۡ أُوتِيتُمۡ هَٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمۡ تُؤۡتَوۡهُ فَٱحۡذَرُواْۚ وَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ فِتۡنَتَهُۥ فَلَن تَمۡلِكَ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔاۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَمۡ يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمۡۚ لَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٞ ﴾
[المَائدة: 41]

Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wa fanyao haraka kukufuru, miongoni mwa wanao sema kwa vinywa vyao: Tumeamini, na hali nyoyo zao hazikuamini, na miongoni mwa Mayahudi, wanao sikiliza kwa ajili ya uwongo, wanao sikiliza kwa ajili ya watu wengine wasio kufikia. Wao huyabadilisha maneno kutoka pahala pake. Wanasema: Mkipewa haya basi yashikeni, na msipo pewa haya tahadharini. Na mtu ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumfitini huwezi kuwa na madaraka naye mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu hataki kuzitakasa nyoyo zao. Watakuwa na hizaya duniani, na Akhera watakuwa na adhabu kubwa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الرسول لا يحزنك الذين يسارعون في الكفر من الذين قالوا آمنا, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الرسول لا يحزنك الذين يسارعون في الكفر من الذين قالوا آمنا﴾ [المَائدة: 41]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wale ambao wanakimbilia kuukanusha unabii wako miongoni mwa wanafiki ambao wameonyesha Uislamu na huku nyoyo zao ni tupu, kwani mimi ni Mwenye kukuokoa na wao. Na lisikuhuzunishe lile la kukimbilia kwa Mayahudi kuukanusha unabii wako, kwani wao ni watu wanaosikiliza urongo, wanayakubali yanayozuliwa na wanavyuoni wao na wanawasikiliza watu wengine wasiohudhuria kwenye baraza yako; na wengine hawa wanayageuza maneno ya Mwenyezi Mungu baada ya kuyaelewa na wanasema, «Yakiwajia kutoka kwa Muhammad yanayolingana na yale tuliyoyageuza na tukayapotosha katika hukumu za Taurati, basi yatumieni. Na yakiwajia kutoka kwake yanayokwenda kinyume na hayo, basi jihadharini kuyakubali na kuyatumia.» Na ambaye Mwenyezi Mungu Ataka apotee, basi hutaweza, ewe Mtume, kulizuia hilo lisiwe kwake na wala huwezi kumuongoza.. Na hakika hawa wanafiki na Mayahudi, Mwenyezi Mungu Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao na uchafu wa ukafiri, wana udhalilifu na fedheha hapa duniani, na watapata, huko Akhera, adhabu kubwa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek