Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 51 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلنَّصَٰرَىٰٓ أَوۡلِيَآءَۘ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَإِنَّهُۥ مِنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[المَائدة: 51]
﴿ياأيها الذين آمنوا لا تتخذوا اليهود والنصارى أولياء بعضهم أولياء بعض ومن﴾ [المَائدة: 51]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mlioamini, msiwafanye Mayahudi na Wanaswara ni washirika na wasaidizi wenu juu ya watu wa Imani. Hii ni kwa kuwa wao hawawapendi Waumini. Mayahudi wanasaidiana wao kwa wao, na hivyo hivyo ndivyo walivyo Wanaswara. Na makundi yote mawili yanakutana kwenye kuwafanyia nyinyi uadui. Na nyinyi, enyi Waumini, mnafaa zaidi kusaidiana nyinyi kwa nyinyi. Na yoyote mwenye kuwategemea wao katika nyinyi, basi yeye atakuwa ni miongoni mwao, na hukumu yake ni yao. Mwenyezi Mungu Hatawaafikia madhalimu wanaowategemea makafiri |