Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 60 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿قُلۡ هَلۡ أُنَبِّئُكُم بِشَرّٖ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيۡهِ وَجَعَلَ مِنۡهُمُ ٱلۡقِرَدَةَ وَٱلۡخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّٰغُوتَۚ أُوْلَٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ ﴾
[المَائدة: 60]
﴿قل هل أنبئكم بشر من ذلك مثوبة عند الله من لعنه الله﴾ [المَائدة: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Nabii, kuwaambia Waumini, «Je, niwajulishe yule ambaye atalipwa, Siku ya Kiyama, malipo makali zaidi kuliko hawa wenye kutoka nje ya utiifu?» Hao ni waliowatangulia wao ambao Mwenyezi Mungu Aliwafukuza kwenye rehema Yake, Aliwakasirikia na akawageuza maumbile yao Akawafanya manyani na ngurue kwa kuasi kwao, kuzua kwao urongo na kuwa na kiburi, kama ambavyo walikuwa kati yao wenye kuabudu Tāghūt (kila kinachoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu nacho kimeridhika). Hao, ni pabaya mno mahali pao huko Akhera; na harakati zao ulimwenguni zilikosa mwelekeo wa njia ya sawa |