Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 61 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿وَإِذَا جَآءُوكُمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَقَد دَّخَلُواْ بِٱلۡكُفۡرِ وَهُمۡ قَدۡ خَرَجُواْ بِهِۦۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا كَانُواْ يَكۡتُمُونَ ﴾
[المَائدة: 61]
﴿وإذا جاءوكم قالوا آمنا وقد دخلوا بالكفر وهم قد خرجوا به والله﴾ [المَائدة: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wakiwajia nyinyi, enyi Waumini, wanafiki wa Kiyahudi husema, «Tumeamini,» na hali wao wako ukafirini na wanaendelea nao : hakika wameingia kwenu wakiwa na ukafiri wanaouitakidi ndani ya nyoyo zao, kisha wametoka wakiwa bado wanaushikilia ukafiri huo. Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa siri zao hata wakionyesha kinyume cha hivyo |