×

Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa 5:8 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:8) ayat 8 in Swahili

5:8 Surah Al-Ma’idah ayat 8 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 8 - المَائدة - Page - Juz 6

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُواْ قَوَّٰمِينَ لِلَّهِ شُهَدَآءَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شَنَـَٔانُ قَوۡمٍ عَلَىٰٓ أَلَّا تَعۡدِلُواْۚ ٱعۡدِلُواْ هُوَ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ ﴾
[المَائدة: 8]

Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا كونوا قوامين لله شهداء بالقسط ولا يجرمنكم شنآن قوم, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا كونوا قوامين لله شهداء بالقسط ولا يجرمنكم شنآن قوم﴾ [المَائدة: 8]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, kuweni wasimamizi wa haki kwa ajili ya kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, muwe mashahidi kwa uadilifu. Wala kusiwapelekee nyinyi kuwachukia watu kuacha kufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu baina ya maadui na vipenzi kwa daraja moja sawasawa. Kufanya uadilifu huko kuko karibu zaidi na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Na jihadharini na kufanya udhalimu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa mnayoyafanya na Atawalipa kwa hayo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek