Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 7 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَمِيثَٰقَهُ ٱلَّذِي وَاثَقَكُم بِهِۦٓ إِذۡ قُلۡتُمۡ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ﴾
[المَائدة: 7]
﴿واذكروا نعمة الله عليكم وميثاقه الذي واثقكم به إذ قلتم سمعنا وأطعنا﴾ [المَائدة: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu katika sheria Yake Aliyowaekea na kumbukeni ahadi Yake Yeye Aliyetukuka, Aliyoichukua kwenu ya kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kuwasikiliza na kuwatii. Na mcheni Mwenyezi Mungu katika Aliyowaamrisha na Aliyowakataza. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayoyaficha katika nafsi zenu |