×

Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo 5:89 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Ma’idah ⮕ (5:89) ayat 89 in Swahili

5:89 Surah Al-Ma’idah ayat 89 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 89 - المَائدة - Page - Juz 7

﴿لَا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ ٱلۡأَيۡمَٰنَۖ فَكَفَّٰرَتُهُۥٓ إِطۡعَامُ عَشَرَةِ مَسَٰكِينَ مِنۡ أَوۡسَطِ مَا تُطۡعِمُونَ أَهۡلِيكُمۡ أَوۡ كِسۡوَتُهُمۡ أَوۡ تَحۡرِيرُ رَقَبَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖۚ ذَٰلِكَ كَفَّٰرَةُ أَيۡمَٰنِكُمۡ إِذَا حَلَفۡتُمۡۚ وَٱحۡفَظُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ ﴾
[المَائدة: 89]

Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru

❮ Previous Next ❯

ترجمة: لا يؤاخذكم الله باللغو في أيمانكم ولكن يؤاخذكم بما عقدتم الأيمان فكفارته, باللغة السواحيلية

﴿لا يؤاخذكم الله باللغو في أيمانكم ولكن يؤاخذكم بما عقدتم الأيمان فكفارته﴾ [المَائدة: 89]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Hatawapa mateso, enyi Waislamu, kwa mayamini mliyoapa bila ya kukusudia, mfano wa vile baadhi yenu wanavyosema, «Sivyo, naapa kwa Mwenyezi Mungu», «Kwa Nini? Naapa kwa Mwenyezi Mungu.» Lakini Yeye Atawapa mateso, kwa sababu ya mayamini mliyoyakusudia ndani ya nyonyo zenu. Basi mkiwa hamtekelezi yamini, dhambi lake litafutwa na Mwenyezi Mungu, kwa kafara mtakayotoa mliyowekewa na Mwenyezi Mungu ya kuwalisha masikini kumi, kila masikini mmoja apewe nusu ya pishi [kadiri ya kilo mbili na nusu] ya chakula cha kati na kati kinachotumiwa na watu wa mji aliyoko, au kuwavisha kwa kumpa kila maskini mavazi yanayomtosha kulingana na desturi, au kuacha huru mmilikiwa kumtoa kwenye utumwa. Basi mwenye kuapa ambaye hakutekeleza yamini lake ana hiari afanye mojawapo ya mambo matatu. Asipopata chochote kati ya hayo, ni juu yake afunge siku tatu. Kufanya hayo ndio kafara ya kutoyatekeleza mayamini yenu. Na yachungeni mayamini yenu, enyi Waumini, kwa kujiepusha na kuapa au kutekeleza kiapo mnapoapa au kutoa kafara msipotekeleza kiapo. Na kama alivyowaelezea Mwenyezi Mungu hukumu ya mayamini na namna ya kujivua nayo, ndivyo Anavyowaelezea hukumu za dini Yake, ili mumshukuru Yeye kwa kuwaongoza nyinyi kwenye njia iliyolingana sawa
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek