Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 97 - المَائدة - Page - Juz 7
﴿۞ جَعَلَ ٱللَّهُ ٱلۡكَعۡبَةَ ٱلۡبَيۡتَ ٱلۡحَرَامَ قِيَٰمٗا لِّلنَّاسِ وَٱلشَّهۡرَ ٱلۡحَرَامَ وَٱلۡهَدۡيَ وَٱلۡقَلَٰٓئِدَۚ ذَٰلِكَ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَأَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ ﴾
[المَائدة: 97]
﴿جعل الله الكعبة البيت الحرام قياما للناس والشهر الحرام والهدي والقلائد ذلك﴾ [المَائدة: 97]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Amewafadhili waja Wake kwa kuijaalia Alkaba, Nyumba takatifu, ni utengenefu wa Dini yao na amani ya uhai wao. Hivyo ni kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakasimamisha faradhi Zake. Na Ameharamisha uadui na kupigana katika miezi mitakatifu (nayo ni Mfungopili, Mfungotatu, Mfungone na Rajabu) ili mtu yoyote asimfanyie mwingine uadui katika miezi hiyo. Na Ameharamisha, Aliyetukuka, kuwavamia wanyama- howa wanaotolewa kuwa ni tunu kwa Haram. Kadhalika, Ameharamisha kuvivunjia heshima qalaid, navyo ni vitu vilivyovishwa shingoni mwa hao wanyama kuonyesha kuwa wanakusudiwa kuchinjwa kwa ibada. Hivyo basi, ni mupate kujua kuwa Mwenyezi Mungu Anayajua yote yaliyo mbinguni na ardhini, miongoni mwayo ni sheria Alizoziweka kuwahami viumbe Wake wasidhuriane wao kwa wao. Na pia mupate kujua kwamba Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi, hakuna chochote chenye kufichika Kwake |